THE GAME YAMKUTA YA R.KELLY, SASA KUKOSA MAPATO YA ALBAMU YAKE IJAYO


Rapper gwiji, 'The Game' yupo kwenye hatari ya kukosa mirahaba yake (Royalties) kwenye album yake ijayo kwa sababu mwanamke anayedai kuwahi kunyanyaswa kingono ameiomba mahakama kufanya hivyo. 

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizodakwa na mtandao wa 'THE BLAST', imearifiwa kuwa Priscilla Rainey amemuomba Jaji kupata haki yake kwa kuchukua haki zote, mirahaba na kwa mapato yoyote atakayopata 'The Game' kwa sasa hasa kupitia album yake ijayo iitwayo 'Born to Rap'. 

Rainey bado anadai fidia ya ($7.2 milioni) sawa na Tsh bilioni 16 ambayo alishinda mahakamani kwenye kesi yake ya kunyanyaswa kingono na 'The Game' wakati wa usaili wa kipindi cha VH1 cha 'The Game' mnamo mwaka 2015. 

Kazi kweli...

Post a Comment

0 Comments