TID:SINA TATIZO NA Q CHILLA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 25, 2019

TID:SINA TATIZO NA Q CHILLA

Staa wa Bongo Fleva, TID amesema kuwa hana tatizo na staa mwenzake Q Chilla na kuwa anashaa akiongelewa vibaya na staa huyo.“Mimi sina tatizo lolote na Q Chilla ila nashangaa yeye anavyokuwa ananiongelea vibaya maana kumuongelea mtu vibaya hakufanyi wewe kuonekana mzuri,” TID alisema.

“Mara ya mwisho nakutana na Q chilla ilikuwa mwezi mmoja uliopita na alivyoniona akanipiga bao, kiukweli sikumuelewa maana hajui nimetumia kiasi gani cha fedha au muda gani kutengeneza brand yangu kisha yeye kutaka kuiharibu, sijui anataka kuniona nimepanga Mwananyamala kama yeye hata sielewi,” TID alisema hayo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Hivi karibuni Q Chilla alinukuliwa na chomno cha habari kimoja akielezea kuwa na tatizo na TID

 "Ni kweli mimi na T.I.D tuna migogoro takribani miaka miwili sasa, nisingependa kuyaongelea sana madhambi ya mwenzangu lakini hata mimi nina mashabiki ambao wananifatilia na wanaona kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yangu na nafikiri kwa watu wenye akili timamu wamefatilia na kugundua nani mwenye matatizo kati yetu", amesema Q Chilla.

No comments: