TP MAZEMBE YAFUNGUKA MAZITO KUHUSU SIMBA

TP Mazembe imemtaja Afisa Habari wa Simba, Haji Manara kuwa ni mmoja wa mashabiki wasumbufu wanapokuwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Katika tovuti ya TP Mazembe imeandika habari kuwa Simba ni timu iliyokosa mchezo wa kiungwana na kuitumia picha ya Manara yenye maelezo huyu ni mmoja wa mashabiki wasumbufu wa Simba.
Katika kuonyesha hofu yao kwa Simba, tayari TP Mazembe imetuma ujumbe kwa CAF ikiwataka kufuatilia kwa karibu mbinu zinazotumiwa na Simba dhidi ya wapinzani wake.
Taarifa hiyo imesema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa timu zilizocheza Dar es Salaam katika hatua mbalimbali za Ligi ya Mabingwa msimu huu yaliyofika CAF.
Nkana, JS Saoura, Al Ahly na Vita Club, wapinzania hao wa Simba wamelalamikia kuhusu kupewa mabasi mabovu, pamoja na kupuliziwa vitu vyenye harufu kali katika basi hayo;
Pia, kumekuwa na matukio ya mashabiki kuwafanyia vurugu timu ngeni wakati wa kwenda kufanya mazoezi pamoja na muda wa kuingia uwanjani siku ya mchezo.
Taarifa hiyo iliendelea ilisema 

‘Pamoja na shutuma zote hizo kwa klabu hiyo ya Tanzania, imethibika kuwa mashabiki wa Simba SC katika siku ya mchezo walijaribu kuzuia msafara wa timu pinzani kuingia katika vyumba kwa kufunga milango ya uwanjani. Jambo la kushangaza pamoja na kufunga milango ya vyumba kwa timu mwenyeji, bado kulikuwa na harufu vyumbani katika siku ya mechi.
Dar Es Salaam, wenyeji wanakuwa si waungwana. Baada ya kuwasili Tanzania jana usiku, TP Mazembe wametuma ujumbe kwa CAF, FECOFA na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu mapungufu hayo. Al Ahly, Saoura na Vita Club wanajua vizuri: walipewa viwanja vibovu vya mazoezi.
Kwa tahadhari hiyo, TP Mazembe hawana la kufanya zaidi ya kuomba uangalizi wa karibu wa CAF. Uongozi wa klabu unataka kupewa ushirikiano kwa asilimia zote kutoka kwa Simba ili mchezo wa Jumamosi uchezwe kwa kuzingatia kanuni za soka, bila ya kuwepo kwa aina yoyote ya vitendo vya vurugu na uvunjifu wa kanuni na sheria.
TP Mazembe ipo tayari kwa ushirikiano wote, baada ya kikao, kwa ajili ya kufanyika kwa mchezo wa kiungwana.

Post a Comment

0 Comments