Uber imezindua kipengele kipya cha kutoa Tip nchini Tanzania


      

Dar es Salaam, Aprili 17, 2019 - Sasa wasafiri wanaotumia mfumo wa Uber wanaweza kutoa tip kwa madereva baada ya safari - hii inatokana na kipengele kipya ambacho kampuni ya Uber imetangaza leo. Kipengele cha kutoa tip kinawapa wasafiri wanaotumia Uber fursa ya kuonyesha shukrani zao kwa huduma nzuri wanayopata kutoka kwa madereva-washirika wa Uber. Pesa zote zitakazotolewa kama tip zitamwendea dereva husika moja kwa moja na hakuna ada yoyote ya huduma
itakayotozwa pesa hizi.
Meneja wa Uber Kusini mwa Jangwa la Sahara  Alon Lits, anaelezea; “Kuendesha gari ni zaidi ya kumtoa msafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Madereva- washirika wanaotumia mfumo wetu wanajituma kila siku, ili kuhakikisha kwamba wanawarahisishia wasafiri wetu shughuli zao za kila siku - kuwafikisha kwenye mikutano muhimu ya kikazi, kuwapeleka nyumbani baada ya shamrashamra za mitoko ya jioni - wanafanya kila aina ya safari. Hii ndiyo maana tumeweka mkazo na tunafanya juhudi endelevu katika kuimarisha huduma zetu.”
“Ujio wa kipengele hiki unatokana na maoni tuliyopokea kutoka kwa madereva- washirika kupitia vikao mbalimbali ambavyo tumekuwa navyo ikiwa ni mkakati wa kuboresha na kuimarisha huduma zetu. Kupitia kipengele hiki, Uber inatoa njia ambayo madereva-washirika, wanaojituma kwa kutoa huduma nzuri kwa wasafiri, watatambuliwa na kutuzwa kwa kazi nzuri wanayoifanya. Madereva kama hawa ni wale husubiria hadi wahakikishe mteja ameingia nyumbani kabla waondoke.” amehitimisha Bw. Lits.
Msafiri kutumia kipengele hiki ni hiari kwa 100% na wasafiri watapewa kiasi fulani ambacho watachagua tip ambayo wangependa kumpa dereva. Kipengele hiiki kitakuwa sehemu ya chini ya tathmini na pongezi ya app. Malipo yote ya tip yatakatwa kwenye kadi ya benki ya msafiri iliyosajiliwa kwenye mfumo wa Uber, kwa wasafiri wanaolipa kwa njia ya keshi wako huru kumpa dereva tip moja kwa moja.  
Hivi ndivyo inavyofanya kazi:
  • Jinsi ya kumpa dereva tip
  • Pakua toleo jipya la app.
  • Mwishoni mwa safari yako, ongeza tip baada ya kutathmini safari yako.
  • Chagua mojawapo kati ya kiasi kilichowekwa au uweke kiasi unachotaka.
  • Bonyeza Nimemaliza ili utume tip yako.
  • Pesa zote za tip zitatumwa kwa dereva moja kwa moja, Uber haitatoza ada
  • yoyote ya huduma kwenye tip.
Kuhusu Uber
Dhamira ya Uber ni kuwasaidia watu kutumia simu ili kupata usafiri - kila mtu na mahali popote. Tulianza mwaka 2009 kwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo dogo: unawezaje kutumia simu yako kuita usafiri? Baada ya kufanya safari zaidi ya bilioni 10, tumeanza kutafuta ufumbuzi wa tatizo kubwa zaidi: kupunguza foleni ya magari na uchafuzi wa mazingira katika miji mbalimbali kwa kutumia magari machache kusafirisha watu wengi. Uber inatoa huduma zake katika miji kumi na tatu Kusini mwa Jangwa la Sahara (Cape Town, Durban, Joburg, Pretoria, Port Elizabeth, Nairobi, Mombasa, Lagos, Abuja, Kampala, Accra, Kumasi and Dar es Salaam). Kwa jumla mtandao wa Uber unapatikana katika miji zaidi ya 600 na zaidi ya nchi 65. Ili msafiri aweze kuita gari, ni lazima aweke app ya Uber ya simu za Android, iPhone, Blackberry 7, au ajiandikishe kutumia Uber kupitiawww.uber.com/go. Kwa maswali tafadhali tembeleawww.uber.com
Kwa Taarifa zaidi:
Janet C. Kemboi - Communications - East Africa
Simu: +254 726 390190
Barua Pepe: jkemboi@uber.com

Post a Comment

0 Comments