VAR YAMALIZA VITA YA MANCHESTER CITY VS TOTTENHAM HOTSPURS - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 18, 2019

VAR YAMALIZA VITA YA MANCHESTER CITY VS TOTTENHAM HOTSPURS

Tottenham Hotspurs inatarajiwa kuvaana na Ajax Amsterdam ya Uholanzi katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Spurs imetinga nusu fainali baada ya kupata ushindi wa kushangaza jana usiku dhidi ya Manchester City.
Licha ya kufungwa mabao 4-3 na Man City, Spurs imesonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini.

Spurs ilishinda bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa kwenye uwanja wake wa Tottenham.

Shujaa wa Spurs alikuwa Fernando Llorente aliyefunga bao la tatu dakika ya 73 na kuipeleka timu hiyo katika nusu fainali.

Hata hivyo, mwamuzi wa mchezo Cuneyt Cakir raia wa Uturuki alizimika kupata msaada wa VAR kujiridhisha kama mfungaji huyo alishika mpira kabla ya kujaza wavuni.

Mchezaji Son Heung-Min raia wa Korea Kusini aliyekuwa mwiba kwa mabeki wa Man City, alifunga mabao mawili ya Spurs dakika ya saba na 10.

Man City iliyokuwa ikipewa nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo ilipata mabao yake kupitia kwa wachezaji Raheem Sterling aliyefunga mawili dakika ya nne na 21, Bernado Silva (11) na Sergio Kun Aguero (59).


“Nashukuru wachezaji wangu na mashabiki walicheza vizuri. Mashabiki walikuwa watulivu sikusikia kelele kutoka kwao, nakubali matokeo lakini tulicheza kwa kiwango bora,” alisema kocha wa Man City Pep Guardiola.

Katika mchezo mwingine wa jana usiku, Liverpool ilifuzu nusu fainali baada ya kuibanjua FC Porto mabao 4-1.

Mwanaspoti
Loading...

No comments: