Venezuela Kuandamana Nchi Nzima Leo


Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido ameitisha maandamano ya nchi nzima leo hii, yaliyopewa jina la 'Operesheni ya Uhuru' ya kumshinikiza Rais Nicolas Maduro kuondoka madarakani.

Kulingana na Guaido, ambaye anatambuliwa na mataifa 50 kama kiongozi wa mpito wa nchi hiyo, maandamano hayo ya miezi kadhaa yanaingia katika awamu ya mwisho.

 Marekani na Colombia ambazo ni miongoni mwa nchi zinazomuunga mkono Guaido, zimemuonya Maduro dhidi ya kumuweka Guaido kizuizini.

Uongozi wa Maduro umelitumbukiza taifa hilo katika mgogoro wa kiuchumi, lakini jeshi bado linamuunga mkono kiongozi huyo na kumuwezesha kung'ang'ania madaraka. 

Post a Comment

0 Comments