VIINGILIO MECHI YA SIMBA VS TP MAZEMBE VYATAJWA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 2, 2019

VIINGILIO MECHI YA SIMBA VS TP MAZEMBE VYATAJWA

TIMU ya Simba imetangaza viingilio vya mchezo wao dhidi ya TP Mazembe mapema leo kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara.Akitangaza vingilio hivyo mbele ya waandishi wa habari, Manara alisema wametangaza mapema bei za tiketi ili kila shabiki achukue mapema kukwepa msongamano siku ya mechi.

Viingilio hivyo  ni kama ifuatavyo; Mzunguko Shilingi Elfu Nne (4000) VIP B Shilingi Elfu Kumi (10,000) VIP A Shilingi Elfu Ishirini (20,000) PLATINUMZ Laki Moja (10,000).

Manara alisema mabadiliko ya bei za tiketi safari hii yametokana na ukubwa wa mchezo kati yao na TP Mazembe, kwanitimu hatua waliyopo ni tofauti na iliyopita.

"Mechi iliyopita tulikuwa tumetoka kupoteza kwahiyo tuliweka kiingilio kile kuwashtua mashabiki wetu, lakini mchezo huu kila mmoja pia anatambua kabisa ukubwa wa timu na hata hatua tuliyopo ndio maana kiingilio cha chini ni Elfu Nne na awali ilikuwa Elfu mbili," alisema.

Mechi ya Simba na TP Mazembe itachezwa  Aprili 6, 2019 siku ya jumamosi kwenye uwaja wa taifa ambao ni mchezo wa kwanza  wa robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika ambayo ni Simba kutoka Tanzania ndiyo muwakilishi pekee kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi ya vilabu barani Afrika.


Loading...

No comments: