WANACHAMA NSSF WAANDAMANA HADI OFISI ZA UBUNGO PLAZA KUDAI STAHIKI ZAO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 30, 2019

WANACHAMA NSSF WAANDAMANA HADI OFISI ZA UBUNGO PLAZA KUDAI STAHIKI ZAONSSF Kinondoni

BAADHI ya wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), walikusanyika jana Jumatatu, Aprili 29, 2019 katika Ofisi za NSSF wilaya ya Kinondoni zilizopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakidai malipo ya stahiki zao.

Wakizungumza na Global TV nje ya ofisi hizo, kwa nyakati tofauti, wanachama hao wameilalamikia NSSF wakisema imeshindwa kuwalipa mafao yao kwa wakati licha ya kukamilisha taratibu zote na kuahidiwa kulipwa, wamedai wamekuwa wakipoteza muda mrefu kufuatilia malipo yao bila mafanikio.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi wa NSSF waliokuwepo, walijifungia ndani ya vyumba vya ofisi hiyo na kugoma kuzungumzia sakata hilo, huku jengo zima la ofisi zao likiwa giza.

Aidha, Meneja wa Mkoa wa NSSF amezungumza na Global TV kwa njia ya simu na kukiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuwa yupo njiani anaeleka ofisini kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na kwamba tatizo kubwa lililokuwepo ni kuharibika kwa miundombinu ya umeme kwa siku kadhaa hadi leo na kusababisha kushindwa kufanya kazi. 

CHANZO: GLOBAL TV
Loading...

No comments: