Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani AjiuzuluWaziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kirstjen Nielsen amejiuzulu jana, kutokana na kile alikiona kuwa ni ukosefu wa uungaji mkono kutoka kwa washirika wa Rais Donald Trump kuhusu idadi ya familia za Kutoka Amerika ya Kati zinazovuka mpaka wa kusini na kuingia nchini humo.

Lwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle (DW), Trump ametangaza jana kwenye mtandao wa Twitter kuwa Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka nchini Marekani Kevin McAleenan atachukua nafasi ya kaimu katika wizara huyo.

McAleenan ni afisa wa muda mrefu wa ulinzi wa mipaka ambaye anaheshimiwa sana na wabunge na ndani ya serikali.


Nielsen alisafiri pamoja na Trump Ijumaa iliyopita kwenda kwenye mpaka wa Marekani na Mexico kushiriki katika mazungumzo na maafisa wa mpakani na polisi wa eneo hilo 

Post a Comment

0 Comments