WEMA AJIONGEZE- MARTIN KADINDA

Meneja wa zamani wa staa wa bongo movie Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema kwasasa Wema ameshakuwa mtu mzima na anaweza kujiongoza mwenyewe hivi haitaji kusimamiwa tena.


Wema Sepetu na Martin Kadinda

Akiongea na EATV  Martin ambaye ni mbunifu wa mavazi hapa nchini  alifunguka;

"Unapokuwa na elimu naamini ni rahisi kufanikiwa kwenye vitu unavyofanya kwakuwa changamoto utazichukulia katika hali chanya, hutokuwa mwepesi wa kukata tamaa, hivyo basi Wema ni mwanadada msomi na anaweza fanya hivyo kwani amekuwa sasa anatakiwa kujiongeza", amesema Kadinda.

Kuhusu uhusiano wake kwasasa na staa huyo, Martin amesema kutoonekana muda mwingi na Wema haimaanisha hawana mahusiano mazuri.

Na kuhusu mwenendo wa Wema amesema kuwa sasa hivi mwanadada huyo anamuona katulia tofauti na awali ambapo alikuwa hakaukiwi matukio.

Post a Comment

0 Comments