WEMA SEPETU ATOA WITO HUU KWA WASANII WENZAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 18, 2019

WEMA SEPETU ATOA WITO HUU KWA WASANII WENZAKE

Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu  amewataka wasanii wenzake kujiwekea malengo yao katika uigizaji  ili kuwa na thamani ambayo itakuja kuwasaidiahata kipindi watakapozeeka.
Wema Sepetu

Akizungumza katika kongamano la waigizaji lililoandaliwa na Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na chamacha waigizaji Taifa lililofanyika jijini Dar es Salaam, Wema alisema ni wakati sasa kwa waigizaji wa kike kujitengenezea thamani katika uigizaji.

Alisema amekumbana na kesi mbalimbali mahakamani na kupotezea muda mwingi alikuwa anahangaikia masuala ya polisi mambo ambayo amedai yametokana nay eye mwenyewe kushindwa kulinda nembo yake.

“Nilifungiwa kazi zangu za uigizaji hiyo ni moja  ya changamoto kubwa ambayo pia ilinikumba , niliumia na kuwa mnyoge kwa sasabu naipenda kazi ya Sanaa kuliko kitu chochote n ayaote haya yalitokana na kutolinda Brand yangu,” alisema Wema.

Alisema ili wasanii waweze kufanikiwa na kutimiza malengo yao katika uigizaji  wanapaswa kuwa na uongozi bora  unaowasimamia kwani utahakikisha na kufanikiwa kupata tenda  na matangazo mbalimbali.

“Niwaeleze wenzangu ukiwa unashirikiana na kitu chochote cha zaida huwezi kuendelea  hata siku moja hivyo tunapaswa kuwa na viongozi wazuri  na kujinasua katika mambo yasiyo na maana kama tumeshajijua sisi ni ‘Brand’ muhimu katika jamii,”alisema.

Alisema ili msanii aweze kufika mbali na kujulikana kimataifa pia muhimu kuepuka matumizi ya dawa za kulevya.
Loading...

No comments: