WEMA SEPETU AVUNJA UKIMYA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA DIANA

Staa mrembo wa Bongo Movie Wema Sepetu,amesema uhusiano wake na muigizaji mwenzake Diana Kimario ni wa ‘UDADA’ na sivinginevyo,  na kuwa yeye atabaki kuwa dada wa msanii huyo kama ilivyo kwa wasanii wengine.

"Mimi nitabaki kuwa dada kwa Diana kama nilivyo kwa Allu au Lulu, wote wale wadogo zangu hakuna kingine", amesema Wema.

Mwanadada huyo ambaye kwasasa ni Balozi wa Startimes, amesema ameshapunguza baadhi ya marafiki wasiofaa na ataendelea kusimama kama dada kwa wadogo zake wengine kwenye tasnia a filamu na nje ya filamu.  

Akizungumzia kuhusu mama yake kuchukizwa na urafiki wake na Diana ambao mama yake alidai hauna faida, wema sepetu alisema mama yake kukasirika ni kawaida na kama mama akichukizwa na mwanaye anatakiwa kuwa hivyo lakini wako sawa.

Post a Comment

0 Comments