WIZI WA MAFUTA YA TRANSFOMA TUTAWACHUKUKLIWA KAMA WAHALIFU WAANOTUMIA SILAHA: KMANDA MAMBOSASA
 KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiwa na Meneja wa Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Maxmillian Birigi, akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya madumu yenye mafuta ya transfoma.
 Meneja wa Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Maxmillian Birigi, akizunhumza
 KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizunhumza na waandishi wa habari
 KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya miundombinu ya TANESCO iliyoharibiwa na wahalifu hao. ikiwa ni pamoja na mashine za kuchomelea za wahalifu hao.
 KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiwa na Meneja wa Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Maxmillian Birigi, akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya madumu yenye mafuta ya transfoma.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameonya kuwa kuanzia sasa mtu yeyote anayehujumu miundombinu ya TANESCO hatabaki salama na polisi itamchukulia kama  muhalifu anayetumia silaha.
Kamanda Mambosasa ameyasema hayo leo Aprili 30, 2019 kwenye Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wake wa pamoja na Meneja wa Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Maxmillian Birigi, baada ya maafisa usalama wa shirika hilo kwa kushirikiana na polisi kunasa mtandao wa wahalifu walioiba kiasi kikubwa cha mafuta ya transfoma ikiwa ni pamoja na vyuma vinavyojenga transfoma jijini Dar es Salaam.
“Madhara wanayosababisha ni zaidi ya uhalifu wa kutumia silaha, kwa sababu wanaharibu uchumi wa nchi, na wanafikia mahali wanaharibu vyombo mbalimbali vinavyotumiwa na wananchi.” Alisema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa alisema Aprili 25, 2019 majira ya saa 5 usiku  jeshi la polisi kwa kushirikiana na maafisa wa usalama wa TANESCO waliendesha operesheni ya kuwasaka watu wanaohujumu miundombinu ya Shirika hilo katika maeneo mbalimbali ya jiji na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 9.
“Mtuhumiwa mmoja akiwa katika ghala la TANESCO lililoko eneo la Kigamboni alikutwa akiiba mafuta kwenye transfoma namba T26840 aina ya TCO ya mwaka 2007.” Alisema.
Mtuhumiwa baada ya kuhojiwa kwa kina, alitaja watuhumiwa wengine nane anaoendesha uhalifu huo na baada ya polisi kuwatia mbaroni walisema mafuta hayo humuuzia mtu mmoja ambaye walisema huyachanganya mafuta hayo na vimiminika vingine kisha kutengeneza mafuta ya oil ambayo huyapa majina ya makampuni mbalimbali ya mafuta yanayouza vilainishi vya mitambo na magari.
“Baada ya kufika kwenye ghala na maduka yaliyo eneo la Tabata Dampo, polisi kwa kushirikiana na maafisa hao wa TANESCO walikamata shehena ya madumu 68 ya lita 20 za makampuni mbalimbali ya mafuta, hata hivyo mshukiwa mkuu anayenunua mafuta hayo alifanikiwa kutoroka na msako wa kumtia mbaroni unaendelea.” Alisema.
Katika upekuzi huo polisi pia walifanikiwa kukamata mapipa mawili yenye ujazo wa lita 200 yakiwa na mafuta ya transfoma.
Katika muednelezo wa operesheni hiyo, Kamanda Mambosasa alisema pia polisi ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na vibati maalum vinavyokaa ndani ya transfoma vinavyosaidia kuzalisha umeme na pia zilikamatwa mashine tano za kuchomelea zilizotengenezwa kienyeji ambazo ni matokeo ya wizi wa vibati hivyo vya transfoma.
“Katika mahojiano walisema vibati hivyo huvitumia kutengenezea mashine za kuchomelea yaani welding machines, wanaeda kuharibu miundombinu ya TANESCO wapate hivyo vipati kwa ajili ya kutengeneza mashine hizo hili hatutakubali.” Aliaapa Kamanda Mambosasa.
KWA upande wake, Meneja wa Usalama na Upelelezi wa TANESCO Bw. Maxmillian Birigi, yeye alisema ili kupata mafuta ya transfoma, lazima uivunje kwanza transfoma yenyewe ili uweze kuyapata mafuta yaliyoko mle ndani.
Transfoma ikiisha mafuta mafuta na kwasababu moto unazidi kuingia lazima ile transfoma ilipuke na kuwaka moto.
“Athari zake kubwa mbili ni pamoja na TANESCO kununua transfoma nyingine ili kurudisha huduma ya umeme kwa wananchi lakini wakati Shirika likifanya jitihada za kurudhisha huduma hiyo, wananchi watakosa huduma ya umeme kwa hivyo mtaweza kuona kwa ksiai gani hawa watu ni wahujumu uchumi kwelikweli kama alivyosema Kamanda Mambosasa.” Alisema Bw. Birigi.
 

Post a Comment

0 Comments