Yaliyojiri kwenye mkutano wa ECOSOC Jijini New-York Vijana wazungumza - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 10, 2019

Yaliyojiri kwenye mkutano wa ECOSOC Jijini New-York Vijana wazungumza
Mkutano wa Vijana wa ECOSOC (Economic and Social Council) uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New-York Marekani umemalizika leo ambapo vijana wameweza kujadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya Elimu, Ajira, Kuchukua hatua kwenye mabadiliko ya tabia ya nchi, Amani na Haki za binadamu. 
Mkutano huu ulifunguliwa na Rais wa ECOSOC, Mrs Inga Rhonda King, alisisitiza kuwa vijana ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo na kujenga jamii yenye amani na utulivu. 
"Vijana wanahitaji "ujuzi, maadili, kazi na maisha ambayo huwawezesha" ili waweze kusaidia kuunda dunia endelevu zaidi. 

Tunahitaji kushughulikia kwa haraka changamoto zinazoelezea wakati wetu: upatikanaji wa elimu bora, ukosefu wa ajira, kutofautiana, kutengwa na jamii na mabadiliko ya hali ya hewa ",  mrs Inga alisisitiza katika maneno yake ya ufunguzi. "Hatuwezi kutatua hizi changamoto  kwa Umoja wa Mataifa pekee. Bali, sisi sote kwa pamoja ".

Dhima kuu ya mkutano wa mwaka huu ni "Uwezeshwaji, Ujumuishwaji na Uwiano", Jukwaa la mwaka huu linalenga kuhamasisha msaada kwa vijana duniani kote.
Wakati akibainisha dalili zenye kuhimiza kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), alielezea ushahidi unaojitokeza ambao unaonyesha "dunia bado haijafikiria kufikia  SDGs nyingi ifikapo mwaka wa 2030".

Tanzania ilipata bahati ya kuwakilishwa na vijana watatu kutoka taasisi tofauti tofauti za vijana hapa. Vijana hawa walipa fursa ya kujadili changamoto na fursa za vijana wa Tanzania na jinsi gani vijana wanaweza kujitolea katika kazi za kijamii. 
Ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika ngazi zote za maamuzi, kusikilizwa na kueleweka, kuchukua hatua na kutekeleza majukumu yao kila siku. Mkutano huu ni fursa ya vijana kukutana kwenye ngazi za maamuzi pamoja na viongozi wa nchi kushirikisha mawazo yao katika kupiga hatua kwenye malengo ya maendeleo endelevu, Addis Abba Action Agenda na Paris Agreement (Makubaliano kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi).
Loading...

No comments: