Yondani Kukosa Mechi Tatu Ligi Kuu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 12, 2019

Yondani Kukosa Mechi Tatu Ligi Kuu


Yondani Kukosa Mechi Tatu Ligi Kuu
Beki wa kikosi cha Yanga SC Kelvin Yondani sasa atakosa jumla ya mechi tatu zijazo katika ligi na faini sh.500,000.

Adhabu hiyo atakumbana nayo kufuatia kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo wa jana dhidi ya Kagera sugar uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-2.

Beki huyo atakosa mechi hizo kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Kagera na kupelekea kulimwa kadi hiyo.
Michezo mitatu atakayoikosa beki huyo kisiki nchini ni dhidi wakata miwa wa Mtibwa Sugar ambao utachezwa Morogoro (17 April 2019) Azam FC vs Yanga (29 April 2019) na Mchezo wa FA dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa Iringa. 
Loading...

No comments: