ZARI AMUWEKA WAZI MPENZI WAKE MPYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 23, 2019

ZARI AMUWEKA WAZI MPENZI WAKE MPYA

Mrembo na staa wa Uganda  aliyewahi kuwa mpenzi wa staa wa Bongo Flevam, Diamond Platinumz, Zari Hassan ametangaza kwamba amepata mpenzi mpya.Mpenzi huyo mpya ambaye amemtaja mpenzi huyo kwa herufi 'M' katika mtandao wake wa Instagram anadai ndiye aliyechukua nafasi ya Diamond.

Akitangaza uhusiano wake mpya katika mtandao huo wa kijamii Zari Hassan alisema kuwa mpenzi wake mpya amemkubali yeye pamoja na watoto wake wote watano.

'Kwako wewe mpenzi nimejifunza mengi; Nakumbatia maisha yalivyo kwa sababu ya unyenyekevu wako. Nimekuwa nikifikiria maisha yangu ya baadaye lakini sikuweza kujua maisha hayo yatakuwa vipi. Watoto watano, wanaume wengine lakini bado ukaniona mimi kuwa mwanamke mrembo zaidi'', alisema Zari katikaandiko lake.

''Nakupenda sana bwana M, na sio vitu vyenye thamani unavyonionyesha, nimeviona hivyo na hata vikuu na vizuri zaidi. lakini ni wewe, moyo wako, uwepo wako na vile unavyotufanya mimi na wanangu kukuhisi. Wewe ni jasiri sana bwana M:

Zari alisema yeye mwenyewe ana miaka 38, na ana watoto watano lakini bwana wake huyo umetumwa kutoka mbinguni mpenzi. Nakupenda bwana M,'' aliongezea Zari katika chapisho hilo.

Mrembo huyo wa Uganda alizungumzia kuhusu nafasi yake katika kujenga maisha ya wapenzi wake wa awali ambao anasema hawakumpenda kwa dhati sambamba na kukemea wanaodai kumjua mpenzi wake mpya.

 
Loading...

No comments: