Ziara ya Rais Magufuli Mkoa wa Njombe Yaongezwa Siku - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, April 6, 2019

Ziara ya Rais Magufuli Mkoa wa Njombe Yaongezwa Siku


Ziara ya Rais Magufuli Mkoa wa Njombe yaongezwa siku
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John pombe Magufuli,anatarajia kufanya ziara ya siku Tatu mkoani Njombe baada ya kutokea mkoani Ruvuma na kukagua baadhi ya miradi mikubwa ikiwemo ya barabara na hospitali.

Akizungumza na vyombo vya habari ofini kwake, mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amesema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli atafanya ziara ya siku Tatu kuanzia tarehe 09-11/04/2019.

Olesendeka amesema kuwa katika Ziara hiyo atatembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo na kuongea na wananchi.

“mheshimiwa Rais siku ya kwanza atapokelewa na viongozi wa serikali, chama pamoja na wananchi katika mpaka wa mkoa wa Njombe na mkoa wa Ruvuma  siku ya tarehe 9 mchana na kwenda katika eneo la uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata chai cha kabambe Tea factory inayomilikiwa na kampuni ya Uniliver  Plc ya London nchini Uingereza  kwa pamoja na kampuni ya Uniliver  nv ya Roturdam nchini Netheland, na kufanya kazi mbili kubwa ikiwemo kuzindua kiwanda hicho na kuzungumza na wananchi watakao kuwepo katika eneo la kiwanda hicho,na baada ya hapo ataondoka kupitia barabara ya Njombe-Songea kwenda katika eneo lake la kupumzika la ikulu ndogo ya Njombe”alisema Olesendeka

Amesema siku ya pili Rais atafanya kazi mbili kubwa ambazo ni kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospital ya Rufaa ya mkoa wa Njombe katika eneo la kutolea huduma za nje (OPD)   uliokamilika kwa asilimia 95 na imegharimu kiasi cha Tshs.Bilioni 3.6

Aidha ataweka jiwe la Msingi katika barabara inayounganisha makao makuu ya mkoa wa Njombe na wilaya ya Makete yaani Njombe -Moronga-Makete  katika eneo la shule ya msingi ya Ramadhani inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya takribani Tshs.Bilioni 217 ikiwa ni moja kati ya miradi ya barabara za lami na zege zinazojengwa mkoani Njombe yenye thamani ya zaidi ya Tshs.Bilioni 480 pamoja na kufanya mazungumzo na wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Ramadhani.

Katika hatua nyingine Olesendeka amesema kuwa,

 “siku ya Tatu ya ziara ya Rais Magufuli ambayo ni tarehe 11 ya mwezi wanne atapata fursa ya kufungua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mafinga-Nyigo -Makambako-Igawa eneo la mpaka wa Makambako na wilaya ya Wanging’ombe ambao ni kilometa 64.6 uliojengwa kwa kiwango cha lami ya kisasa na kugharimu Tshs.Bilioni 103,432,947,407.64 na baadaye katika eneo hilo la makambako atapata fursa ya kuzungumza na wananchi wa miwili watakao kuwa wamehudhuria katika uzinduzi wa mradi huo wa barabara”alisema Olesendeka

Kutokana na umuhimu wa ziara hiyo Olesendeka ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa jirani ya Mbeya na Iringa kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo miradi itazinduliwa pamoja na mikutano ya hadhara ili kumlaki na kumsikiliza Rais na kiongozi huyo wa kitaifa. 
Loading...

No comments: