ABBAH 'AMMAINDI' HANSTONE KWA KUGOMA KUTOKEA KWENYE VIDEO YA 'CHIBONGE' - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 3, 2019

ABBAH 'AMMAINDI' HANSTONE KWA KUGOMA KUTOKEA KWENYE VIDEO YA 'CHIBONGE'


Mtayarishaji wa Muziki nchini "Abbah Process" amesema kitendo cha msanii Hanstone kugomea kuonekana kwenye video ya wimbo wake mpya "Chibonge" ni kumkosea heshima na kutotambua thamani yake kwani yeye ndiye aliyemfanya afahamike.

Kugomea kwa Hanstone kuonekana kwenye Video kulimfanya Abbah kuifanyia remix kazi yake na kumshirikisha G-Nako kufanikisha adhma yake ya kutoa video. 

"Nilimtafuta Hanstone mara kadhaa hakupokea simu yangu ikabidi nimtumie kiongozi wangu lakini bado ilishindikana, kwani alieleza kuwa uongozi wake umemzuia kuonekana kwenye video yangu na ndipo nikachukua jukumu la kufanya remix" alisema. 

Aliendelea kusema kuwa; "Hanstone ni mdogo wangu wala hakutakiwa kufanya hivyo kwani mimi ndiye niliyegundua kitu kutoka kwake mpaka hao wengine wakamuona" 

Kazi yake ya "Chibonge' ni mwendelezo wa kazi mbalimbali ambazo mtayarishaji huyo wa muziki nchini ameenelea kuzifanya baada ya "Chombo ya Fundi" ft. Mesen Selekta. 

Loading...

No comments: