ARUSHA: SERIKALI YATAIFISHA MALI ZA WAKILI MWALE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 6, 2019

ARUSHA: SERIKALI YATAIFISHA MALI ZA WAKILI MWALE


Serikali imetaifisha rasimi Mali za Wakili maarufu Nchini Median Mwale zenye thamani ya Tsh bilioni 1.2 zilizotokana na zao la utakatishaji mara baada ya mahakama kuu kumtia hatiani na kuamuru Mali hizo zitaifishwe.

Akiongea katika zoezi la makabidhiano kati ya ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP na Hazina,Mkurugenzi wa Mashtaka , (ASP )Biswalo Mganga alizitaja Mali hizo kuwa ni pamoja na Magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa kituo kikuu cha polisi,jijini hapa.

Mali zingine zilizotaifishwa ni pamoja na Nyumba mbili ikiwemo iliyopo ploti Namba 261 block c Njiro na nyumba nyingine iliyopo ploti namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.


Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia mahakama kuu kanda ya Arusha, kutaifisha Mali hizo na kwamba April 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaifisha rasimi na kuwa Mali ya serikali.

"Kwa mujibu wa sheria Mali zinapotaifishwa kuwa Mali ya serikali zinakuwa chini ya katibu mkuu Hazina" Alisema.

Naye kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa Mali za serikali Hazina,Benezeth Rutta Alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa wizara ya fedha zinapangwa kadri serikali itakavyoona inafaa.

"Mali hizi Mara baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana Mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada" Alisema Rutha.

Kwa upande wake kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi ,Selemani Nyakulinga Alisema Alisema kuwa mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dolla la marekani milioni 17.2 kutoka mfuko wa global fund kwa ajili ya kusaidia kutibu malaria na HIV Nchini Tanzania zikitoka kwenye Hazina ya nchi ya Marekani.

Alisema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni RAIA wa Kenya wakishirikiana na watanzania akiwemo Wakili Median Mwale .

Alisema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua Mali mbalimbali zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama iliamuti na kutaifisha Mali hizo kuwa mali za serikali. 

Loading...

No comments: