Ukweli wa Ishu ya Askofu Gwajima Kujulikana Leo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 8, 2019

Ukweli wa Ishu ya Askofu Gwajima Kujulikana Leo

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Jumatano Mei 8, 2019 anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kanisani kwake Ubungo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kuhusishwa na video ya ngono.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima

Taarifa hiyo imekuja kufuatia kusambaa kwa video ikimuonyesha mtu anayedhaniwa ni yeye akiwa faragha na mwanamke.

Taarifa yake iliyotolewa kupitia Kituo cha Redio Clouds FM leo asubuh, imeeleza kuwa askofu atazungumza na waandishi wa habari ila ajenda itakayozungumziwa itajulikana wakati huo.

Jana baada ya kusambaa kwa video hiyo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa alinukuliwa akisema tayari wameshamwita Gwajima kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu video hiyo.

“Tayari askofu Gwajima ameitwa polisi kwa ajili ya kuhojiwa na ataripoti kesho (leo) asubuhi , akichelewa atakamatwa na tumemuita sababu hakuna aliyelalamika lakini tumeona ni kitendo cha ukiukwaji wa maadili, awe askofu awe mtu wa kawaida ule ni unyama, “amesema Mambosasa
Loading...

No comments: