BAADA YA TANZANIA, SASA MATANGAZO YA BETTING YAPIGWA MARUFUKU KENYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 2, 2019

BAADA YA TANZANIA, SASA MATANGAZO YA BETTING YAPIGWA MARUFUKU KENYA


Bodi ya kusimamia michezo ya kubashiri (Betting) ya nchini KENYA leo imepiga marufuku matangazo ya kuhamasisha michezo hiyo kuonekana (kurushwa au kutangazwa) kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku. 

Aidha, matangazo hayo yamezuiwa kutangazwa mitaani, kwenye runinga na mitandao yote ya kijamii kwa wakati huo uliotajwa ili kupunguza wimbi la vijana wengi ambao huacha kufanya kazi na kwenda kubashiri nchini humo. 

Barua yenye maelekezo ya kusitisha matangazo hayo ya Betting nchini Kenya.
Ukiachana na matangazo kukatazwa, Watu mashuhuri/watu maarufu wamezuiwa kutumika kuhamasisha michezo hiyo pia. 

Pamoja na michezo hiyo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa serikali kutokana na kodi kubwa sana inazotoa kila mwaka, madhara yake yamezidi kuonekana sana hasa kwa vijana wengi na wanafunzi ambao huacha kuhudhuria masomo kikamilifu na kujikita katika kucheza michezo hiyo. 

Vijana wakipanga 'mikeka' yao tayari kwa kubet
Michezo hiyo imekuwa kivutio kikubwa sana kwa vijana wengi wanaopenda michezo na kutumika kwa watu maarufu kwenye kuitangaza kumeongeza mvuto zaidi kwa wananchi kuicheza. 


Loading...

No comments: