Membe Amjibu Rostam, Urais 2020 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 17, 2019

Membe Amjibu Rostam, Urais 2020

Waziri mstaafu wa Mambo ya Nje wa serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe amemjibu mfanyabishara Rostam Aziz kuhusu suala la kugombea urais 2020 akimtaka hivi sasa ajikite kwenye masuala ya kitaifa yanayohusu uchumi.
Bernard Membe


Jana Mei 16, 2019, picha moja ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Rostam akizungumzia suala la urais 2020 na kumshauri Membe asijitokeze kuwania nafasi hiyo badala yake aachiwe Rais John Magufuli kwa awamu nyingine.
Akizungumza muda mfupi baada ya kutoka mahakamani jijini Dar es Salaam leo Mei 17, 2019, Membe ambaye mwaka 2015 alijitosa kwenye mbio za kuwania urais, amesema Rostam hapaswi kuzungumzia mambo yanayomhusu mtu mmoja kwa sababu kwa taaluma aliyonayo ni vyema akasaidia katika mambo ya kitaifa.
“Napata kigugumizi mno kumjibu rafiki yangu Rostam, lakini Rostam ni mchumi na nitakutana naye nimshauri kuwa anafanya vizuri sana katika jamii ya Watanzania yanapozungumziwa masuala ya uchumi. Inabidi azungumze main issues za nchi, siyo personal, hizi tunaachia watu wa chini, level zetu ni kuzungumzia masuala ya kitaifa ya uchumi.
"Kwanini uchumi wetu upo hapa ulipo, kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao au zile alizozieleza kama vikwazo vya uchumi ni vipi na tunajikwamua vipi.

“Rostam ni mchumi hivyo angejikita katika eneo hilo kwa kuwa anafanya vizuri upande huo na asijaribu wewe ni mwenzetu sisi tumekatwa mkia, ukikatwa mkia hata ujitahidi vipi mkia wako utabaki kuwa mfupi. Tuwe tunazungumza kwenye dhamira zetu yawe sawa na yale tunayozungumza mdomoni, tuwe tunazungumza kitu ambacho binadamu watatuheshimu," amesema.
Loading...

No comments: