BOBI WINE AACHIWA HURU KWA DHAMANA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 3, 2019

BOBI WINE AACHIWA HURU KWA DHAMANA

Uganda politics

Mwanamuziki na Mwanasiasa wa nchini Uganda Bobi Wine ameachiwa kwa dhamana jana Mei 2 baada ya kukaa siku 3 kwenye jela ya Luzira nchini Uganda.

Akiwa gerezani kwenye ulinzi mkali Bobi Wine alisomewa dhamana hiyo huku akionekana kwenye video baada ya zoezi la kufika mahakamani kushindikana kutokana na kuhofia usalama.

Bobi Wine ambaye anatuhumiwa kwa mashtaka ya kuandaa maandamano 'haramu' kwa ajili ya kupinga kodi ya mitandao (OTT) amekana mashtaka yote dhidi yake. 

Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki aliachiliwa kwa kulipa dhamana ya kiasi cha fedha dola 265. 

Loading...

No comments: