EBOLA YAUA ZAIDI YA WATU 1000 CONGO DRC - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 6, 2019

EBOLA YAUA ZAIDI YA WATU 1000 CONGO DRC


Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema zaidi ya watu 1,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini humo. 

Shirika la afya duniani WHO limesema hali mbaya ya usalama, uhaba wa fedha na kauli za wanasiasa zinazowachonganisha wahudumu wa afya na raia zimeathiri kwa kiasi kikubwa juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji wa kitengo cha dharura cha WHO Michael Ryan ametahadharisha kwamba maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yataendelea. 

Ryan amesema chanjo dhidi ya ugonjwa huo zipo lakini hazitoshi na kwamba zaidi ya watu 110,000 wameshapewa chanjo tangu kulipuka kwa maradhi hayo. 

Nchi jirani za Rwanda na Uganda pia zinaendelea na zoezi la kuwachanja wahudumu wake wa afya. 

Loading...

No comments: