HATIMAYE MISS MBEYA 2019 APATIKANA, APEWA BODABODA YAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 6, 2019

HATIMAYE MISS MBEYA 2019 APATIKANA, APEWA BODABODA YAKE

Hatimaye Mshindi wa shindano la ulimbwende kwa mkoa wa Mbeya (Miss Mbeya 2019) amepatikana. 

Miss Mbeya
Miss Mbeya 2019 Angela Deocress akiwa na zawadi yake ya pikipiki aliyozawadiwa  kama mshindi wa shindano hilo.
Shindano hilo lililofanyika usiku wa tarehe 3 pale Tughimbe Hall, Mafyati Mbeya, liliweza kumtoa Angela Deocress kuwa mshindi wa taji la miss Mbeya kwa msimu huu.

Angela alishiriki mashindano ya mwaka jana (Miss Mbeya 2018) na kuishia kwenye kumi bora lakini mwaka huu karudi kwa kishindo na kujipanga zaidi na kuwashinda wengine wote. 

Aliyeibuka mshindi wa pili ni Nelly ambaye alikuwa miss Mbeya mwaka jana, na mshindi wa tatu alikuwa ni Evangelina Peter ambaye naye mwaka jana alifanikiwa kuingia tano bora. 

Miss Mbeya 2019
Miss Mbeya 2019 Angela (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wenzie
Mshindi amezawadiwa pikipiki mpya Aina ya TANHERO ambayo Ina uwezo wa kumpatia kipato na hata kutimiza Ndoto zake, waandaji ametoa pongezi kwake na Shukrani kwa wanambeya kwa kushirikiana kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa tukio
 
Kuhusu kupewa zawadi ya Pikipiki, Mshindi Angela alisema anashukuru kwani zawadi ni Zawadi, sababu ukubwa wa Zawadi unategemeana na uwezo wa muandaaji. Kwake yeye amesema ni fursa kwani anaenda kujulikana kitaifa na kimataifa. Ndoto yake ni kuwa Miss Tanzania. Kwasasa anachowaza ni Mashindano yaliyo mbele yake na si Zawadi. Kawashukuru Waandaaji pia.

Pikipiki mpya aina ya TANHERO ambayo iliandaliwa kama zawadi ya mshindi wa Miss Mbeya 2019

Ikumbukwe kuwa mashindano hayo huandaliwa na kituo cha redio cha Dream FM kila mwaka kutoka mkoani Mbeya. 

Loading...

No comments: