ZIJUE HATUA 6 ZA KUACHANA NA MPENZI WAKO VIZURI

Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuachana kwa ugomvi.

Mshauri wa mahusiano Gabriel Jackson akizungumza kwenye DADAZ ya EATV ametoa dondoo zifuatazo ambazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani.

1. Mwambie unahitaji kuzungumza naye. Hapa kuna watu wanashindwa kuzungumza matokeo yake wanatuma meseji tu naomba tuachane, kufanya hivyo katika mahusiano sio sahihi.

2. Mwambie mazuri yake. Unapokuwa umemuita na kuitikia wito basi anza kwa kumwambia mazuri yake, mpe sifa zake na mshukuru kwa yote aliyokufanyia kipindi cha mahusiano yenu.

3. Mwambie waziwazi sasa nataka tuachane.

4. Mpe sababu za kuachana. Usimfiche chochote na usijidanganye wala kukubali kuwa mpeane muda, muda wanapeana wanandoa.

5. Mpe nafasi ya kuzungumza na yeye anachojisikia badala ya wewe kuzungumza.

6. Mpe moyo, mshauri na mueleze sifa zake na mwambie anaweza kupata mpenzi mwingine.


Post a Comment

0 Comments