IGP SIRRO: "TUTAFUATILIA YOTE YANAYOSEMWA KUHUSU KIFO CHA DKT MENGI" - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 6, 2019

IGP SIRRO: "TUTAFUATILIA YOTE YANAYOSEMWA KUHUSU KIFO CHA DKT MENGI"

IGP Simon Sirro akitoa pole kwa wafiwa katika msiba wa Dkt Mengi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi lake litafuatilia kwa kina maneno yote yanayosemwa mitandaoni kuhusu Kifo cha Reginald Mengi ili kubaini kama yanaukweli wowote ili sheria ichukue mkondo wake.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo baada ya kufika nyumbani kwa Dr Mengi ili kutoa Pole ya msiba.

"Mzee Mengi alikuwa mshauri mzuri sana kwenye masuala ya ulinzi na usalama pamoja na misaada midogo midogo kwa vijana wetu wanapokuwa na shida. Zaidi alikuwa ‘very humble’ mara zote alikuwa anajishusha sana.

"Yako mengi yanayoongelewa kwa sasa mitandaoni, lakini jambo la msingi tumalize kwanza msiba, hayo yanayozungumzwa mitandaoni tutafuatilia," amesema Sirro. 

No comments: