Uwoya Afungukia Kuitwa ‘Sista’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 13, 2019

Uwoya Afungukia Kuitwa ‘Sista’

STAA mrembo wa Bongo movie, Irene Uwoya amefunguka kwamba, alipokuwa akisoma sekondari alikuwa akivaa sketi ndefu mpaka chini kitendo kilichosababisha wanafunzi wenzie wampe jina la sista.


Uwoya amesema kuwa wakati ameanza kidato cha kwanza alikuwa mpole sana, wazazi wake wakamshonea sketi za shule ndefu mpaka mguuni kiasi ambacho wenzie walikuwa wakimtania na kumuita sista na kwa wakati huo alikuwa akiona kawaida tu.

“Yaani huwezi amini mtu akiniletea zile sketi leo naweza nisimuelewe kabisa na nitamshangaa sana, lakini mimi nilikuwa nazivaa wenzangu wananitania na kuniita Sista Irene", amesema Uwoya.
Loading...

No comments: