JAMBAZI SUGU NA KADA MAARUFU WA CCM ARUSHA AKAMATWA

Jumanne Mjuzi
Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia jambazi sugu Jumanne Mjuzi (J4) mkazi wa Ngarenaro jijini Arusha ambaye pia ni kada maarufu wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kosa la kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo bastola moja yenye risasi tisa.

Jambazi huyo maarufu kwa kutambaa kwenye kuta za nyumba za watu anapokuwa akitekeleza uhalifu huo, alikamatwa Mei 16 mwaka huu Majira ya saa 11 jioni baada ya kuvamia na kuvunja nyumba ya mkazi mmoja wa eneo la Olasiva anayejulikana kwa jina la Msafiri Msuya

Kamanda wa polisi Mkoani hapa,ameeleza vyombo vya habari kuwa jambazi huyo alifanikiwa kupora kiasi cha shilingi milioni 6 ,Laptop na bastola aina ya Browning ikiwa na risasi tisa zilizokuwa kwenye begi Mali ya Msafiri Msuya.

"Baada ya kupata taarifa hiyo jeshi la polisi kupitia askari wenye weredi walifanikiwa kufanya msako na ndani ya masaa 48 tulifanikiwa kumtia mbaroni mhusika pamoja na vitu alivyopora"Alisema Kamanda.

Jambazi huyo miaka ya nyuma aliwahi kukimbilia bungeni kwa nia ya kujisalimisha baada ya Polisi kuwa wanamsaka kutokana na matukio ya uhalifu yaliyokuwa akitekeleza jijini Arusha na baada alikiri makosa akiapa kutorejea makosa yake na kujiingiza kwenye chama cha mapinduzi kama kivuli cha uhalifu.

Hata hivyo Mara chache amekuwa akikamatwa akihusishwa na matukio ya uporaji na kufikishwa kituo cha polisi na baadae kuonekana mtaani,huku akidai kuwa amestaafu ujambazi .

Jamanne Mjuzi alikuwa kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye alishiriki kwenye chaguzi mbalimbali za marudio kama kiongozi wa kikosi maalumu cha ulinzi aliyekuwa akihusishwa kuwakata mapanga wafuasi wa chadema na kupelekea baadhi yao kupata ulemavu wa kudumu. 

Post a Comment

0 Comments