LIVERPOOL WAPITIA MAGUMU WALIYOYAPATA UNITED CAMP NOU, MESSI AWEKA REKODI MPYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 2, 2019

LIVERPOOL WAPITIA MAGUMU WALIYOYAPATA UNITED CAMP NOU, MESSI AWEKA REKODI MPYA


Wahenga walisema "ukiona mwenzio ananyolewa, za kwako tia maji". Huu msemo mashabiki wa Liverpool unawahusu mno kwani katika mechi yao ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya nusu fainali dhidi ya FC Barcelona iliyopigwa pale uwanja wa Camp Nou. 

Katika mechi hiyo Liverpool wamejikuta wakipokea kichapo cha mabao 3-0 yaliyowekwa wavuni na Luis Suarez dakika ya 26, na Lionel Messi aliyefunga magoli mawili dakika ya 75 na 82 kukamilisha kifo cha majogoo wa Uingereza. 


Wiki mbili nyuma, Manchester United walikwenda Camp Nou katika hatua ya robo fainali ya ligi hii hii na kuambulia kipigo cha 3-0 pia huku Lionel Messi akifunga goli 2 pia. Mashabiki wa Liverpool waliwacheka sana Manchester United bila kujua kuwa na wao yatawakuta. 

Katika mchezo huo pia mshambuliaji na nyota wa FC Barcelona Lionel Messi alifikisha jumla ya magoli 600 katika ngazi ya vilabu akimfikia mpinzani wake aliyepo Juventus Cristiano Ronaldo ambaye naye alifikisha goli 600 wikiendi iliyopita. No comments: