MAAJABU YA USIKU WA ULAYA YAENDELEA, TOTTENHAM WAPINDUA MEZA UHOLANZI


Klabu ya Tottenham Hotspurs ya jijini London, jana usiku iliushangaza ulimwengu kwa kufanya COMEBACK ya kihistoria kwao katika ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kushinda kwa mabao 3-2 ugenini dhidi ya klabu ya AJAX ya nchini Uholanzi na kutinga fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo. 

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliofanyika katika uwanja mpya wa Tottenham pale London, AJAX walishinda 1-0 dhidi ya wenyeji Spurs na kuwapa hali ngumu kuelekea mchezo wa marudiano ambao ndio uliopigwa hapo jana. 

Walikuwa ni AJAX waliotawala kipindi cha kwanza na kujipatia magoli mawili katika kipindi cha kwanza kupitia kwa kapteni wao beki Matthijs DeLigt dakika ya 5, na Hakim Ziyech dakika ya 35. Mpaka mapumziko, AJAX 2-0 Tottenham.

Wakati Ulimwengu ukiamini kuwa mchezo huo umeisha na Ajax wamepita hatua hiyo, Spurs walirudi na morali kubwa sana na kutengeneza nafasi nyingi ambazo zilizaa matunda. 

Winga LUCAS MOURA alikuwa shujaa wa mechi hiyo hapo jana kwa kufunga magoli 3 (Hatrick), dakika ya 55, 59, na 96. Magoli yakafanya matokeo kuwa 3-2 katika mechi hiyo na jumla kuwa 3-3 ukichanganya na matokeo ya mechi ya kwanza pale London. 

Kwa matokeo hayo, Spurs wanaungana na wenzao kutoka Ligi kuu ya Uingereza, timu ya Liverpool ambao nao wameingia fainali juzi baada ya kumfunga Barcelona 4-0. 

Baada ya miaka zaidi ya 6 sasa, kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya litarudi Uingereza baada ya kuchukuliwa na wahispania na wajerumani kwa muda mrefu. 

Tupe utabiri wako, NANI ATAKUWA BINGWA wa ligi ya mabingwa Ulaya? 

Post a Comment

0 Comments