Magufuli Awaongoza Mamia Kumuaga Mengi Dar - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, May 7, 2019

Magufuli Awaongoza Mamia Kumuaga Mengi Dar

Rais wa Tanzania, John Magufuli ameungana na mamia ya waombolezaji katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.Pamoja na Rais Magufuli kuhudhuria shughuli hiyo leo Jumanne Mei 7, 2019, viongozi wengine waliohudhuria pia Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, viongozi wastaafu, viongozi wa dini, kisiasa na watu mbalimbali.

Awali, SheIkh wa Mkoa wa Dar es Salaama, Alhad Musa Salum amewataka Watanzania kumuenzi Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 akiwa Dubai, Falme za Kiarabu kwa vitendo kutokana na mambo mema aliyoyafanya kwenye jamii wakati wa uhai wake.

Amemtaja Mengi kama muasisi wa kamati za amani za mikoa na siku zote alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha amani, upendo na utulivu vinaendelea kutawala.

Kwa upande wake, Askofu Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Nelson Kisare amewataka viongozi kutumia nafasi walizonazo kubadili maisha ya Watanzania kwa kutumia rasilimali zilizopo Tanzania.

Familia ya Dr. Mengi ikiusindikiza mwili wa mpendwa wetu kwa ajili ya kuagwa katika ukumbi wa Karimjee.
Loading...

No comments: