MAN CITY MABINGWA EPL, WAAFRIKA WANG'AA TUZO ZA MFUNGAJI BORA, HAZARD&VAN DIJK WACHEZAJI BORA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 13, 2019

MAN CITY MABINGWA EPL, WAAFRIKA WANG'AA TUZO ZA MFUNGAJI BORA, HAZARD&VAN DIJK WACHEZAJI BORA

Jana ilikuwa ni siku ya kuhitimisha mechi za Ligi kuu ya nchini Uingereza maarufu kama EPL na cha kustaajabisha ni kuwa hadi bingwa aliamuliwa kutokana na mechi za jana pia. Klabu za Manchester City na Liverpool ndio ambazo zilikuwa zikishindana nani abebe ubingwa na hatimaye Manchester City ya Pep Guardiola ndio iliyofanikiwa kushinda mchezo wao na kuibuka mabingwa kwa mara ya pili mfululizo chini ya kocha Pep Guardiola.Katika mbio za kuwania ufungaji bora wa ligi hiyo pamoja na zawadi ya kiatu cha dhahabu, waafrika watatu wamefungana na wote wakapewa viatu vyao kila mmoja. Sadio Mane wa Liverpool Fc (Senegal), Mohamed Salah wa Liverpool Fc (Misri), na Piere Emerick Aubameyang wa Arsenal Fc (Gabon) wote walimaliza msimu wakiwa na magoli 22 kila mmoja wao. Upande wa pili, tuzo ya mchezaji mwenye assist nyingi msimu huu imekwenda kwa Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard ambaye amemaliza msimu akiwa na assist 15.Tuzo ya mchezaji Bora wa ligi hiyo imekwenda kwa beki wa Liverpool, Vigil Van Dijk ambaye amekuwa chachu ya mafanikio makubwa uwanjani kwa klabu ya Liverpool tokea asajiliwe msimu uliopita kutoka klabu ya Southampton. 


Loading...

No comments: