MANCHESTER UNITED RASMI WAJITOA TOP 4, CHELSEA WAING’OA SPURS - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 6, 2019

MANCHESTER UNITED RASMI WAJITOA TOP 4, CHELSEA WAING’OA SPURS

Rasmi, Manchester United hawatacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya pointi zao walizokusanya msimu huu kwenye Ligi Kuu England hazitoshi kuwafanya kuingia ndani ya Top Four.

Sare ya 1-1 ugenini kwa Huddersfield imefuta ndoto zao za Man United kumaliza ligi ndani ya Top Four kwa sababu sasa wamekusanya pointi 66 na wamebakiza mchezo mmoja tu, ambao hata wakishinda wataishia kukusanya pointi 69, moja nyuma ya Tottenham waliopo kwenye nafasi ya nne.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Chelsea wamepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kuibuka na ushindi mtamu kabisa wa 3-0 dhidi ya Watford uwanjani Stamford Bridge.
Wapambanaji wengine wa Top Four ni Arsenal ambao jana usiku walilazimishwa sare 1-1 na Brighton kwenye uwanjani Emirates matokeo hayo ya kikosi hicho cha Unai Emery unafanya vita hiyo ya Nne Bora kusubiri hadi mechi za mwisho kwa timu hizo tatu, Spurs, The Blues na The Gunners.

Loading...

No comments: