MANYARA: MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA BASI LA MTEI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 15, 2019

MANYARA: MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA BASI LA MTEI

Ajali Manyara


Basi la Kampuni ya Mtei lililokuwa likitoka Babati kuelekea jijini Dar es Salaam limegongana na basi dogo katika eneo la Himiti mjini Babati

Inadaiwa kuwa Mwanafunzi wa Shule ya msingi Silver ya mjini Babati ndiye aliyefarika katika ajali hiyo

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Silver mjini Babati mkoani Manyara, amefariki dunia baada ya kutokea ajali kati ya basi la Kampuni ya Mtei kugongana na basi dogo aina ya Hiace.

Ajali Mtei

Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara, Augostino Senga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo asubuhi ya leo Mei 15, 2019 katika eneo la Himiti mjini Babati na kumtaja mwanafunzi aliyefariki kuwa ni Osiligi Paul mwenye umri wa miaka mitatu na miezi mitano.

Kamanda Senga amesema ajali hiyo imehusisha basi la Scania Kampuni ya Mtei na basi dogo aina ya Hiace.

Amesema mwalimu wa Shule ya Silver ambayo zamani ilikua ikiitwa Deborah, Francis Mollel (36) amejeruhiwa kwenye ajali hiyo pamoja na mwanafunzi Lightness Emmanuel (6) na wakala wa Mtei Paul Shilala (28) wamepata majeraha na wapo Hospitali ya Mrara mjini Babati.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la Mtei kuipita gari nyingine bila tahadhari na kugongana na basi dogo kwenye barabara hiyo ya Babati-Kondoa.

"Dereva wa basi dogo, Daniel Godfrey (25) naye alijeruhiwa miguuni yupo Hospitali ya Mrara akipatiwa matibabu ila dereva wa basi la Mtei alikimbia na tunamtafuta, amesababisha ajali kwa uzembe wake,’’ amesema Kamanda Senga. 

Loading...

No comments: