Mbunge Sugu Ataja Jina la Mtoto, Jay-Z Atajwa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 16, 2019

Mbunge Sugu Ataja Jina la Mtoto, Jay-Z Atajwa

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina Sugu kwa furaha leo ametangaza kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram kuwa mtoto wao wa kiume na amemuita la Shawn Joseph Mbilinyi, uchaguzi wa jina la Shwan amedai pia linatokana na kukubali harakati za msanii wa marekani Shawn Carter maarafu kama Jay-Z.


"Tumempa mtoto wetu jina Shawn Joseph Mbilinyi...SHAWN (Tamka SHON) lina maana ZAWADI TOKA KWA MUNGU ( A GIFT FROM GOD)...Pia ni katika kumuenzi Msanii na Mfanyabiashara maarufu duniani Jay-Z, ambaye jina lake halisi ni SHAWN CARTER... Hii ni kutokana na jinsi FALSAFA zake kuhusu HUSTLING zilivyonisaidia kufika hapa nilipo kwenye maisha. Asanteni sana..." Sugu ameandika. 

Sungu ambaye pia ni msanii wa miondoko ya kizazi kimya na mchumba wake Happiness walibahatika kumpata mtoto huyo usiku wa kuamkia siku ya jana tarehe 15.
Loading...

No comments: