MKE WA GWAJIMA AVUNJA UKIMYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 8, 2019

MKE WA GWAJIMA AVUNJA UKIMYA

Grace mke wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amevunja ukimya na kufungukia sakata la video ya ngono inayosambaa ikimuonyesha mtu mwenye sura inayofanana na mumw wake huyo akiwa faragha na mwanamke ambaye bado hajafahamika.

Grace mke wa Gwajima


Akizungumza  wakati Gwajima akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabari kuhusu video hiyo na kueleza kuwa si yake, Grace amesema anafahamu ukweli wa video hiyo na kamwe haiwezi kumyumbisha kwa maelezo kuwa anamfahamu vyema mumewe.
“Mimi ni kama simba, ukweli naufahamu, namfahamu mume wangu na kumuamini na ukweli huo hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.”
“Nipo pamoja na yeye na nitasimama na yeye. Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayeweza kuwa juu yetu,” amesema Grace.
Wakati Grace akizungumza mamia ya waumini wa kanisa hilo walionekana wakimshangilia na kuruka ruka kwa furaha.
Loading...

No comments: