MKURUGENZI WA UDART NA MKEWE WAKAMATWA TENA. WAFUNGULIWA KESI MPYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 16, 2019

MKURUGENZI WA UDART NA MKEWE WAKAMATWA TENA. WAFUNGULIWA KESI MPYA

Robert Kisena

Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar (UDART), Robert Kisena na mkewe, Frorencia Mshauri Membe na wenzao watatu wameunganishwa katika kesi ya uhujumu uchumi wakikabiliwa na mashtaka 19 likiwamo la kuisababisha UDART hasara ya Tsh. Bilioni 2.4

Watano hao wameunganishwa pamoja katika kesi hiyo leo Mei 15, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile na Wakili wa Serikali, Grolia Mwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Washtakiwa hao waliokuwa wakikabiliwa na kesi mbili tofauti kufutiwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba na Rwizile

Aidha, baada ya kusomewa mashitaka hayo mapya, Washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kuahirishwa hadi Mei 28, 2019

Loading...

No comments: