M'MAMA' AMUIBUKIA CHRIS BROWN NYUMBANI KWAKE ILI AONDOE LAANA ALIYOMPA MWANAE


Ni kawaida na imezoeleka kuwa Mama mzazi ndiye hutoa radhi kwa mwanae na ikampata, lakini mwanamke huyu ametoa kali ya mwaka!

Usiku wa Jumamosi Mei 4 mwaka huu Chris Brown alitembelewa nyumbani kwake Tarzana California na mwanamke mmoja toka mjini Texas ambaye alikuja na mwanae wa Kiume akidai kuwa Breezy aliwahi kumlaani.

Walinzi walipiga simu polisi na kuripoti tukio hilo punde walifika na kumkuta akirusha Biblia kwenye ukuta wa nyumba ya staa huyo wa R&B. Baada ya polisi kumuuliza alisema kuwa amefika hapo kuondoa laana aliyopewa mwanae na Chris Brown hivyo kuitundika Biblia ukutani itasaidia kuifuta laana hiyo.

Polisi walihitimisha kwa kusema Mama huyo hayupo vizuri kiakili (mentally unstable) na alichukuliwa kwa ajili ya tathmini na mwanae alipelekwa rumande. Wakati tukio hilo linatokea Breezy hakuwepo ndani, alikwenda kwenye birthday party ya rapper Desiigner. 

Post a Comment

0 Comments