MOI ATAKIWA KULIPA KSH. BILIONI 1.6 KWA KUNYAKUA SHAMBA LA MJANE

Raisi Kenya

Rais mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi ameamriwa na Mahakama Kuu jijini Nairobi amlipe fidia ya Ksh bilioni 1 Susan Cheburet Chelungui na mwanawe David Chelungui kwa kosa la kutumia mamlaka yake vibaya na kuwanyang'anya shamba familia hiyo mnamo mwaka 1983

Mjane huyo aliporwa shamba lake kwa njia ya udanganyifu huku maafisa wakuu Serikalini wakitumiwa katika ndanganyifu huo na kisha kuliuza shamba hilo kwa kampuni ya Rai Plywood (K) Limited

Mahakama ilisema kuwa mbali na Rais Moi, sehemu ya shamba hilo pia iligawiwa kwa aliyekuwa Waziri msaidizi kwenye utawala wa Moi, Stanley Metto

Jaji Ombwayo alisema hakukuwa na ushahidi wowote kuonesha uhalali wa Rais huyo mstaafu kusajiliwa kama mmiliki halali wa shamba hilo. 

Post a Comment

0 Comments