MPOTO KUTEMBEZA WATU PEKUPEKU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, May 7, 2019

MPOTO KUTEMBEZA WATU PEKUPEKU

Mwanamuziki Mrisho Mpoto maarufu Mjomba anatarajia kuzindua ‘Mapinduzi ya Kimkakati’, kila Mtanzania atakayehudhuria uzinduzi atatakiwa kuingia bila kuvaa viatu.

Mrisho Mpoto


Mjomba alisema Mapinduzi ya Kimkakati ni ajenda kubwa ambayo itahusu watu wengi wanaomuishi muasisi wa Tanzania, mwalimu Julias Nyerere lakini hawafanyi ambayo aliyafanya miaka 20 kabla na baada ya kufa kwake.

Alisema mwalimu Nyerere alizikwa chini ya ardhi kwa hiyo siku ya tukio kila ambaye atafika kuungana naye anatakiwa kutovaa viatu, kwani huo ni utamaduni wa Watanzania uliokuwa ukitumiwa na wazee.

“Ningeomba bila kujali nyadhifa au nafasi yako katika jamii siku ya tukio tunatakiwa wote kufika tukiwa pekupeku na leo (jana) ndiyo nimefanya uzinduzi wa jambo langu hilo hapa Mwananchi Communications Limited". Mpoto aliyasema hayo aliyasema jana alipotembelea Makao Mkuu ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

“Bila kuficha nimefurahi sana mkurugenzi mtendaji wa MCL, Francis Nanai kuelewa na kuungana nami katika harakati yangu hii,” alisema Mpoto.

Pia, alisema kutakuwa na uzinduzi wa nyimbo itakayohusu ajenda ya Mapinduzi ya Kimkakati na kutakuwa na zawadi nyingi zitakazotolewa na Nanai.

kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Francis Nanai,” alisema Mpoto.

“Baada ya uzinduzi wa hili la Mpango wa kimkakati tunataka kuona kila Mtanzania anapata walau muda wa kuishi na kuyafanya yale ambayo alikuwa akiyafanya Nyerere kabla na baada ya miaka 20, nafahamu si rahisi jambo hili kueleweka kwa haraka likini kadri siku zinavyozidi kwenda naimani wananchi watafahamu juu ya hilo,” alisema.

“Lakini mbali ya hilo ikumbukwe tafiti zinaonesha kutembea pekupeku ni sehemu ya afya kwani unyayo unapogusana na ardhi moja kwa moja inaongeza siku za kuishi na katika kusoma kwangu hilo lilichangia wazee wetu kuishi kwa muda mrefu zaidi hapa duniani kuliko vizazi vya wakati huu,” alisema Mpoto ambaye aliongezea kuwa watu wataelewa zaidi baada ya uzinduzi ambao bado siku ya rasmi ya kufanyika haijapangwa bao. </div>
Loading...

No comments: