Mwanzilishi wa WikiLeaks afungwa Uingereza - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 1, 2019

Mwanzilishi wa WikiLeaks afungwa UingerezaMwanaharakati, Julian Assange alikamatwa na polisi wa Uingereza Aprili 11, 2019 baada ya maofisa wa ubalozi wa Ecuador kuwaita polisi wamkamate baada ya kuishi ndani ya ubalozi huo kwa miaka saba.
London, Uingereza. Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange amehukumiwa kifungo jela cha wiki 50 baada ya kupatikana na hatia ya kuruka dhamana nchini Uingereza.
Assange amehukumiwa kifungo hicho leo nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kuruka dhamana na kukimbilia ndani ya ubalozi wa Ecuador mjini London mwaka 2012 akipinga kurejeshwa nchini Sweden anakokabiliwa na kesi ya ubakaji na pia Marekani anakokabiliwa na kesi ya udukuzi.
“Ulikuwa na uamuzi na kitendo ulichochagua kufanya ilikuwa ni kuvunja sheria,” alisema jaji Deborah Taylor alipokuwa akisoma hukumu.
Taylor aliendelea kusema: “Hukujisalimisha kwa utashi wako, haukuja kwa hiyari yako hapa mahakamani.”
Mwanaharakati huyo alikamatwa na polisi wa Uingereza Aprili 11, 2019 baada ya maofisa wa ubalozi wa Ecuador kuwaita polisi wamkamate baada ya kuishi ndani ya ubalozi huo kwa miaka saba.

MWANANCHI
Loading...

No comments: