MWILI WA MENGI UMEWASILI DAR - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 6, 2019

MWILI WA MENGI UMEWASILI DAR

Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi umewasili leo mchana Jumatatu Mei 6, 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.


Mwili wa mfanyabiashara huyo umewasili ukiwa katika ndege ya Emirates ukitokea Dubai, Falme za Kiarabu na kupokewa na mamia ya wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali.

Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi Mei 2, 2019.

Kesho mwili wa mfanyabiashara huyo utaagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na utapelekwa nyumbani kwake Kinondoni na Jumatano Mei 8, 2019 utasafirishwa kuelekea kijijini kwake Nkuu, Machame mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika Alhamisi Mei 9, 2019.Loading...

No comments: