MZOZO VENEZUELA: MAREKANI YAPENDEKEZA NGUVU ZA KIJESHI KUTUMIKA KUUTATUA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 2, 2019

MZOZO VENEZUELA: MAREKANI YAPENDEKEZA NGUVU ZA KIJESHI KUTUMIKA KUUTATUA


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema nchi hiyo iko tayari kutumia nguvu za kijeshi kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Venezuela. 

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Foxnews cha nchini Marekani, Pompeo amesema Rais Donald Trump amekuwa wazi kwamba Marekani inaweza kuchukua hatua za kijeshi ikiwa zitahitajika. 

Hata hivyo amesema kuwa Marekani ingependelea suluhisho la kisiasa, ambapo Rais Maduro ataondoka na kuruhusu kuandaliwa kwa uchaguzi mpya. 

Katika mahojiano mengine, mshauri mkuu wa Rais Trump kuhusu masuala ya usalama wa taifa, John Bolton, amekiambia kituo cha CNN kuwa Pompeo atazungumza na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, juu ya hali inavyoendelea nchini Venezuela. Bolton ameishutumu Urusi kuwa kizingiti cha mabadiliko ya nchi hiyo. 

Shutuma hizo zilitolewa pia na waziri Pompeo, aliyedai kuwa kabla ya kujiingiza kwa Urusi, Maduro alikuwa tayari kukimbilia nchini Cuba. 

Loading...

No comments: