Haya Ndiyo Malengo ya Nandy

Staa mrembo anayetikisa anga la Bongo Fleva kwa sasa, Nandy ameweka wazi malengo yake ya kufanya show uwanjani.
Nandy

“Malengo yangu ni kuja kufanya show kwenye uwanja mkubwa, show ambayo nimeiandaa mimi mwenyewe naamini kila kitu kina muda wake na sio mbaya kujaribu kufanya kitu hivyo naamini nitafanya show kwenye uwanja siku moja na naamini nitajaza au hata kama nisipojaza lakini nitakuwa tayari nimejua nguvu yangu ipo wapi” Nandy alieleza.

Mbali na mziki Nandy pia amekuwa akiigiza kwenye tamthilia maarufu ya Huba.

Post a Comment

0 Comments