MIMI NA NINI TUMEACHANA-NAY WA MITEGO

Staa wa Bongo Fleva Nay wa Mitego, a,mefunguka kuwa ameshaachana na msanii mwenzake Nini ambaye walikuwa wapenzi kwa kipindi kifupi. Akioongea na EATV Nay amesema ''Mimi na Nini tumeachana, sipo naye tena muda mrefu nina mahusiano yangu mengine na yana utulivu sana. Mimi huwa sijifichi ila kwasasa nimetulia na mwanamke kama wimbo wangu mpya unavyosema Nishaachaga''.

Nay ameongeza kuwa kwasasa anaangalia zaidi familia yake wakiwemo watoto wake kwani wameshakuwa wakubwa hivyo kuna baadhi ya mambo lazima aachane nayo. 

 

Post a Comment

0 Comments