NDUGAI AMSIMAMISHA MASELE UWAKILISHI BUNGE LA AFRIKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 16, 2019

NDUGAI AMSIMAMISHA MASELE UWAKILISHI BUNGE LA AFRIKA

Ndugai na Masele
Spika Ndugai pamoja na mbunge Masele katika picha ya pamoja.

Spika wa bunge mh Ndugai amesema kwa kutumia mamlaka aliyonayo amemsimamisha mbunge Masele kuliwakilisha bunge la JMT katika bunge la Afrika.

Ndugai amesema Masele amekuwa mtovu wa nidhamu na mwenye tabia za hovyo hovyo na amekuwa akilichonganisha bunge na serikali kwa kupeleka maneno ya uongo na umbea selikalini.

Barua kwa Masele:


Kadhalika Ndugai amesema bunge kwa kutumia kanuni zake ilimteua kampuni ya ukaguzi ya Mangesho kumkagua CAG na tayari kampuni hiyo imemaliza kazi na ripoti zimewasilishwa bungeni.

Ripoti hiyo itawasilishwa kwenye kamati ya hesabu kwa utendaji zaidi.

Spika amesema miaka yote CAG amekuwa akikagua wengine lakini yeye hakaguliwi lakini safari hii mambo ni tofauti kabisa kwani hakuna taasisi isiyopaswa kukaguliwa. 

Loading...

No comments: