NYOKA MWENYE MACHO MATATU AONEKANA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 3, 2019

NYOKA MWENYE MACHO MATATU AONEKANA

Maofisa wa wanyama pori wamesambaza picha za nyoka mwenye macho matatu aliyepatikana katikati ya barabara kaskazini mwa Australia.Shirika la huduma kwa wanyama pori na bustani za wanyama, Northern Territory Parks and Wildlife Service, wameeleza kumshangaa nyoka huyo ambaye picha zake zilisambaa kwa wingi katika mitandao ya kijamii.

, Nyoka huyo aina ya chatu ambaye amepewa jina la Monty Python, alifariki wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa mwezi Machi.

Wataalamu wanasema jicho la tatu la nyoka huyo lililo juu ya kichwa chake lilionekana kuwa ni mabadiliko ya asili.

Maafisa walimgundua nyoka huyo katika mji wa Humpty Doo, kilometa 40 kusini mashariki mwa Darwin.

Nyoka huyo alikuwa na urefu wa inchi 15 na alikuwa akipata taabu kula chakula kutokana na ulemavu wake, maafisa wamenukuliwa na BBC.

Shirika hilo la huduma kwa wanyama pori limesema picha za X-ray zimeonyesha kwamba nyoka huyo hakuwa na vichwa viwili kwa pamoja, badala yake alionekana kuwa na fuvu moja la kichwa na jicho la ziada linalofikisha macho matatu yanayofanya kazi sawasawa," lilieleza kwenye Facebook.

Mtaalamu wa nyoka, Profesa Bryan Fry amelieleza BBC kuwa mabadiliko ya maumbile ni sehemu ya kawaida ya kuumbwa.

"Kila mtoto hupitia mabadiliko ya kiwango fulani - huyu alishuhudia mabadiliko yasio ya kawaida," alisema Profesa Fry, kutoka chuo kikuu cha Queensland.

"Sijaona nyoka mwenye macho matatu awali, lakini umeona chatu mwenye vichwa viwili katika maabara yetu - ni aina tofauti ya mabadiliko kama tunavyoona kwa pacha wachanga wanaozaliwa wameungana."

Ameashiria kwamba huenda jicho hilo la tatu likawa " sehemu ya mwisho ya pacha wa nyoka huyo aliyefyonzwa".
Loading...

No comments: