MAMBO SABA USIYOYAFAHAMU KUHUSU BILIONEA REGINALD MENGI

Taifa la Tanzania limekumbwa na majonzi baada ya kumpoteza mfanyabiashara maarufu ambaye ni mmojawapo wa watu matajiri zaidi barani Afrika.

Reginald Abraham Mengi

Hata hivyo ni wachache wanaojua alichopitia mfanyabiashara huyo kabla ya kuwa mtu tajiri hadi kifo chake.

Haya hapa ni mambo saba ambayo marehemu alipitia na kuyafanya katika maisha yake.
1. Alilala sakafuni

Safari ya maisha ya Bw. Mengi ilianzia eneo la Machame huko Kilimanjaro katika familia masikini ambapo kwa kutokuwa na uwezo wa kifedha, ngozi kavu ya ng'ombe ndiyo ikawa kitanda chake.

Wazazi wake walikuwa wakulima na kuasema kwamba elimu ya msingi kuhusu ujasiriamali aliitoa kwa mama yake.

Mengi anasema mama yake alikuwa akichukua mkungu wa ndizi na kurudi nyumbani na kilo ya mchele mara nyengine alichukua kuku mmoja pekee na kurudi na mfuko wa viazi.

Mara nyingi alichukua mikungu ya ndizi na kuja na sare ya shule.

2. 'Alitoroka Shule'

Alipokuwa kidato cha tano nchini Tanzania alipata fursa ya kusomea uhasibu katika chuo kikuu huko Glasgow nchini Uskochi na kutokana na usiri wake mkubwa hakumuelezea mwalimu wake mkuu kwamba ameshinda ufadhili wa masomo huko Uskochi.

Kwahiyo alitoroka shule licha ya kila mtu kujaribu kumshawishi kukaa.
3.Aliwahi kuwa kondokta wa basi

Alipokuwa shuleni huko Glasgow, mengi alibadilisha mawazo kwa kile alichosomea kwa kuwa hakutaka kuwa karani tena.

Wadhamini wake walisema kuwa alifaa kusalia uskochi kwa miezi sita kwa kuwa walikuwa wamelipia karo muda huo wote.

Alikaa lakini aliwacha masomo na badala yake akaamua kumalizi masomo ya mbele akisoma usiku tu huku wakati wa mchana akifanya kazi nyingi kutoka kuwa kondakta wa basi hadi kuwa mfanyakazi wa usafi.

4.Alijiuzulu saa chache baada ya kupewa kazi Kenya

Baada ya kumaliza masomo yake alirejea Tanzania mwaka 1971 na kuajiriwa na Coopers & Lybrand kampuni ambayo kwa sasa inafahamika kama PricewaterhouseCoopers (PwC).

Alipanda hadi kufikia cheo cha juu kabisa na pia kupata ithibati ya kuwa mwanachama wa taasisi ya uhasibu wa Uingereza na Wales.

Baada ya miaka tisa Mengi alihamishwa hadi ofisi ya Nairobi lakini baada ya saa chache tu akiwa Kenya alijiuzulu.
5.Alikuwa na bidii ya mchwa

Alisema "nilitamani kurudi Tanzania licha ya kujua kwamba ningetajirika iwapo ningesalia Uingereza."

"Lakini nilitaka kurudi nyumbani ili kuwafanyia kitu watu wangu."

Alifanya kazi kwa bidii na akiwa na umri wa miaka 30 alikuwa mmoja wa washirika wadogo sana katika shirika hilo la Coopers & Lybrand.

Ni bidii hiyo hiyo ndiyo ilimsukuma katika ujasiriamali kwa kuanzisha msururu wa makampuni mwanzoni mwa miaka ya 90 mpaka kufikia utajiri wa zaidi ya dola milioni 560 kama ilivyokadiriwa na jarida maarufu la fedha la Forbes mwaka 2014.
6. Aliulaumu mfumo wa Ujamaa Tanzania na kuanza kuuza kalamu

Katika mahojiano yaliochapishwa na jarida la Forbes Afrika Mengi alisema kuwa ndoto yake ilikuwa kuendesha biashara kubwa na kwamba aliulaumu mfumo wa ujamaa kwa kuwa uliua wajasiriamali.

Katika 1980 kulikuwa na uhaba mkubwa kutokana na serikali kuendeleza sera ambazo zilipendelea bidhaa za ndani.

Ulikuwa uhaba huo huo ambao ulimfanya bwana Mengi kwenda katika biashara miaka 1980.

Akiunda na kuuza kalamu. Alikuwa akiagiza vifaa kutoka Kenya na kutengeza kalamu hizo chumbani mwake.

Biashara hiyo ya kalamu ndio iliokuwa mwanzo wake wa kuingiza dola milioni moja.

7. Mara ya kwanza alikataliwa na Jacqueline Ntuyabaliwe

Mengi anasema haikuwa rahisi kumpata mkewe, kwani mara ya kwanza alipotaka kuonana naye wakiwa Ulaya alikataa.

Anasema aliendelea kumfuata na waliporudi nchini Tanzania ndipo wakaonana na penzi likaanza kunoga.

Mengi anasema kuwa iwapo asingekuwa na mpenzi huyo labda angekuwa amefariki kitambo.

katika kitabuu chake I can , I must, I will, Mengi anamzungumzia mrembo huyo kama aliyeleta mwangaza maishani mwake.

"Ananipenda , ananipikia, hufua nguo zangi ka mikono yake mwenyewe na sio mashine, amnaniheshimu na anatambua nafasi yangu kama mwanamume, pia anatambua nafasi yake kama mwanamke."

Post a Comment

0 Comments