REMY MA AACHIWA KWA DHAMANA, KESI YAKE KUSIKILIZWA TENA MAY 24 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 3, 2019

REMY MA AACHIWA KWA DHAMANA, KESI YAKE KUSIKILIZWA TENA MAY 24


Remy Ma aachiwa huru toka rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa masaa kadhaa baada ya kujisalimisha polisi jana Jumatano. Akisindikizwa na mwanasheria wake, Remy Ma alishtakiwa kwa kumshambulia mtu na unyanyasaji.

Akiwa kizimbani leo, mwanasheria wake amemtetea mteja wake kwa kusema sio kweli kama Remy Ma alimshambulia mwanadada Brittney Taylor kwani wakati tukio hilo la kupigwa usoni ukumbini linatokea, alikuwa nyumbani akimnyonyesha mtoto wake mwenye miezi minne.

Mumewe Papoose na rapper Fat Joe ni miongoni mwa waliofika mahakamani, baada ya kulipa dhamana Remy Ma ameachiwa na kesi yake imetajwa kusikilizwa tena May 24.
Loading...

No comments: